Diana Nalubega asimulia wanayopitia wasanii wa kike

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa kike nchini Uganda Dianah Nalubega amezungumza kuhusu mambo wanayokumbana nayo wasanii wa kike katika tasnia ya muziki nchini Uganda hususan kusumbuliwa na watu wanaowataka kingono.

Katika mahojiano Dianah alifichua kwamba alipopata umaarufu kiasi kama mwanamuziki, alikumbana na mashabiki matajiri, mameneja, wasanii wenza na hata maafisa wa serikali waliokuwa wanammezea mate.

Alipoulizwa jinsi msanii anaweza kushughulikia hali hiyo Dianah alisema kwamba inategemea na mtu binafsi kwa sababu watu kama hao ni wengi sana.

“Kuna waziri mmoja hata aliniandikia nyimbo za mapenzi. Nilikuwa nacheka tu. Watu kama hawa hawana ajenda wanataka tu kukutumia.” Alisema msanii huyo.

Dianah alifichua pia kwamba alikuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa wanaume ambao walitaka kuwa kwenye mahusiano naye lakini anasema alijizuia kuingilia maisha kama hayo na badala yake akaangazia kujenga taaluma yake.

Nalubega amekuwa akiimba tanu utotoni lakini aliingilia muziki rasmi kama taaluma mwaka 2011. Yeye ni mtoto wa tano kati ya watoto saba wa Jane na jasper matovu.

Website |  + posts
Share This Article