Jackline Wolper amwomba mumewe msamaha

Wolper alikuwa ametangaza kwamba wameachana na Rich mitindo na sasa wamerudiana.

Marion Bosire
2 Min Read

Jackline Wolper ambaye ni mwigizaji nchini Tanzania amemwomba mume wake Rich Mitindo msamaha. Hii ni baada yake kutangaza siku chache zilizopita kwamba wametengana na wanaendeleza mchakato wa talaka.

Mama huyo wa watoto wawili alichapisha video inayomwonyesha akiwa na wanawe wawili na baba yao Rich na kuandika “Najua mambo mengi yanatokea au yametokea lakini kubwa ni kwamba wewe ni baba wa wanangu, na wanangu wanakuangalia kama shujaa wao.”

Alimtaka Rich amsamehe kwa sababu alifanya alilolifanya kutokana na hasira, “Maisha lazima yaendelee mume wangu nisamehe pale ninapokuwa nakosea na kufanya maamuzi kwa sababu ya hasira, lakini pia nimekusamehe kwa kila kitu.”

Wolper aliendelea kusifia uhusiano wao ambao alisema ni wa kipekee na maelewano kati yao ndiyo ya muhimu. “Najua moyo wako na ninajua bond yetu ni ya kipekee jinsi tunavyoelewana ndio jambo la muhimu kwangu,nashukuru kwa kuwa wewe ni Mume wangu na ninaamini Mungu alikuwa na sababu zake alipopanga mimi na wewe tuwe mwili mmoja.”

Alisisitiza kwamba amemsamehe Rich ambaye huwa anamrejelea kama Baba P “kwa yale yote yaliyopita na pia Mungu asituache maana Mungu kwetu ni kila kitu bila yeye.”

Yapata wiki nne zilizopita, Wolper alichapisha taarifa ndefu kwenye Instagram ambapo alisema kwamba yeye na Rich walikuwa wametengana na akashukuru wote ambao walikuwa na mazoea ya kumpa taarifa kuhusu mwenzake na mienendo yake.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *