Kim Kardashian amtetea binti yake North

Marion Bosire
2 Min Read

Kim Kardashian amechukua hatua ya kumtetea binti yake aitwaye North wa umri wa miaka 12 baada ya mwonekano wake kusababisha minong’ono mitandaoni.

North alionekana akiwa amesukwa nywele ndefu za rangi ya samawati, akiwa na michoro bandia usoni, kipini kwenye pua na vyuma kwenye meno.

Picha na video za mtoto huyo Kim na mwanamuziki Kanye West zilichapishwa kwenye akaunti ya Tiktok na alikuwa na marafiki wake ambao pia walikuwa na mwonekano sawia.

Katika kumtetea, Kim alisema hulka ya North ni ile inayotarajiwa kutoka kwa mtoto wa umri wa miaka 12 akisema kwamba hata yeye akiwa umri huo alijaribu mwonekano huo.

Tofauti kati yake na North anasema ni kwamba wakati huo hakukuwa na mitandao ya kijamii na wazazi wake hawakuwa watu maarufu.

Alihimiza wakosoaji waangazie mambo yanayowahusu, maneno yaliyoungwa mkono na baadhi ya wafuasi wake mitandaoni.

Hii sio mara ya kwanza North anakosolewa mitandaoni kuhusiana na mavazi yake na mwonekano kwa jumla. Mwezi Agosti, alionekana kwenye picha akiwa na mamake nchini Italia.

Wakati huo alikuwa amevaa sketi fupi na akiwa ametoboa shimo kwenye kidole.

Baba ya msichana huyo Kanye West aliwahi kulalamikia tabia zake za ki-utu uzima ilhali ni mtoto ambapo alidai kwamba mwanawe anatumiwa na mamake kuendeleza ushawishi mitandaoni.

Wakati huo alielezea kwamba alikuwa amemkataza Kim asimruhusu North kuchapisha chochote kwenye mitandao ya kijamii lakini bado anaruhusiwa kuchapisha.

Website |  + posts
Share This Article