Butere Girls na St. Anthony Boys ndio mabingwa kitaifa wa soka ya shule za upili

Dismas Otuke
1 Min Read

Shule ya Wasichana ya Butere kutoka Magharibi ya Kenya na shule ya wavulana ya St. Anthony kutoka Kitale ndio mabingwa wa kitaifa wa mashindano ya shule za upili kwa wasichana na wavulana mtawalia kwenye fainali zilizoandaliwa hii leo Jumamosi katika uwanja wa Bukhungu kaunti ya Kakamega.

Mabinti wa Butere walitwaa taji ya kitaifa baada ya kuwavua ubingwa Wiyeta Girls kutoka Tranz Nzoia walipowazaba bao moja kwa bila kwenye fainali.

St. Anthony maarufu kama The Solidarity Boys walipata ushindi wa mabao mawili kwa nunge dhidi ya Dagoretti Boys ya Nairobi, Aldrine Kibet akipachika goli moja kila kipindi.
Ilikuwa mara ya sita kwa St. Anthony kunyakua taji ya kitaifa.

Judith Akumu alipachika goli pekee na la ushindi kwa Butere Girls wakiwaangusha Wiyeta.

Butere Girls

Timu tatu bora kila fani zitashiriki mashindano ya Afrika Mashariki nchini Rwanda baadaye mwezi Agosti.

Kenya itaandaa mashindano ya mwaka ujao ya kitaifa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *