Bunge kupitisha bajeti kwa taasisi huru za Kiserikali nchini

Aidha, Wetangúla alisifia mchango wa NCIC kwa kuleta maridhiano na mshikamano wa kitaifa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangúla amekariri kuwa bunge hilo litapitishia bajeti kwa taasisi huru za kiserikali.

Akizungumza Jumatano afisini mwake alipotembelewa na Mwenyekiti wa tume ya maridhiano na mshikamano wa kitaifa (NCIC), Kasisi Dkt. Samuel Kobia, Wetang’ula ameahidi kuwa bunge litapitisha bajeti za taasisi muhimu nchini, ikiwemo IEBC.

Aidha, Wetangúla alisifia mchango wa NCIC kwa kuleta maridhiano na mshikamano wa kitaifa.

Spika aliitaka NCIC kutoegemea upande wowote katika masuala yanayolikabili taifa kwa sasa.

Website |  + posts
Share This Article