Bukedea, Cheptil na Kimilili zanga’aa FEASSSA

Boniface Musotsi
2 Min Read

Shule za Bukedea (UG), Cheptil na Kimilili zimetawazwa mabingwa wa Soka, Voliboli na handiboli mtawalia katika mashindano ya Afrika Mashariki baina ya shule za upili (FEASSSA) yaliyokamilika ijumaa hii mjini Kakamega.

Bukedea waliebuka wahindi baada ya kuwalaza Musingu magoli mawili kwa moja katika fainali iliyosakatwa ugani Moi mjini Kisumu.

Hii ni mara ya kwanza kwa kwa timu hizo kutinga fainali ya mashindano hayo na kunyakua taji hilo lenye hisia na ushindani mkali.

Awali, ngarambe hiyo iliratibiwa kugaragazwa uwanjani Bukhungu mjini Kakamega ila ikahamishiwa Kisumu kufuatia kisa cha mashabiki kuingia uwanjani wakati wa nusu fainali baina ya Musingu na St.Joseph (JOBO) pale Bukhungu na kupelekea mchuano huo kutibuka.

Kwenye Kitengo cha vipusa, St.Noa (UG) walivishwa taji hilo ilipoipiku Kawempe Muslim (UG) goli moja kwa sufuri nayo Archbishop Njenga ikamaliza ya tatu kwa kuilaza Amus College (UG).

Vile vile, Amis yabil na Nabenye Agnes wa Bukedea na St.Noa mtawalia walituzwa kama wachezaji bora.

Nao Cheptil ni mabingwa wapya kufuatia ushindi wa seti tatu kwa mbili dhidi ya Namugongo (UG).

Bukedea walimaliza wa tatu.Taji hilo pia lilituzwa wasichana wa Kwanzanze waliowapiku Kesogon huku Bishop Sulumeti wakiridhika na nafasi ya tatu.

Kwenye fani hii, Opoya William na Mercy Nabwire wa Namugongo na Kwanzanze mtawalia waliebuka wachezaji bora.

Kwa upande wa Kimilili na Warembo wa Kamusinga, walivuna mataji hayo kwa kuzilemea Adegi (RW) na Namugongo Katika fainali Huku Highway na St.Joseph zikimaliza za tatu mtawalia.

Makala ya 23 yataandaliwa mwaka ujao mjini Morogoro nchini Tanzania.

Boniface Musotsi
+ posts
TAGGED:
Share This Article