Banyana yamtafuna Mwitaliano na kutinga raundi ya pili Kombe la Dunia kwa vidosho

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Afrika Banyana Banyana kutoka Afrika Kusini wametoka nyuma na kuwapiga Italia almaarufu Le Azzuri, magoli 3-2 na kufuzu kwa raundi ya 16 bora fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake.

Mchuano huo uliokuwa wa mwisho wa kundi G uliosakatwa ugani Sky mjini Wellington-New Zealand mapema leo Jumatano.

Kiungo Arriana Curaso aliwaweka Waitaliano kifua mbele kwa goli la dakika ya 11 kupitia mkwaju wa penalti kabla ya Benedetta Orsi kujifunga kunako dakika ya 32 huku kipindi cha kwanza kikiishia sare.

Hilda Magaia alitanua uongozi wa Banyana Banyana dakika ya 67 akiunganisha pasi ya Thembi Kgatlana kabla ya kushirikiana tena wakati Kgatlana alipompokeza pasi Magaia na kubusu nyavu dakika ya pili ya ziada.

Ushindi huo umeipa Afrika Kusini  ushindi wa kwanza katika historia na kuwa timu ya kwanza ya taifa hilo kufuzu kwa raundi ya 16 bora ya Kombe la Dunia.

Banyana Banyana wanajiunga na Super Falcons ya Nigeria katika raundi ya pili ya Kombe la Dunia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *