Agnes Jebet Ngetich atamba Miami

Medina Eisa wa Ethiopia amemaliza wa pili kwa muda wa dakika 14 sekunde 25.92,akifuatwa na mwenzake Herut Meshesha kwa dakika 14 sekudne 40.46.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya kilomita 10 Agnes Jebet Ng’etich amesajili muda wa pili wa kasi ulimwenguni aliposhinda mbio za mita 5,000, katika siku ya kwanza ya mashindano Grandslam Track mjini Miami akisajili dakika 14 sekunde 25.80.

Medina Eisa wa Ethiopia amemaliza wa pili kwa muda wa dakika 14 sekunde 25.92,akifuatwa na mwenzake Herut Meshesha kwa dakika 14 sekunde 40.46.

Baada ya kushiriki mikondo miwili ya Jamaica na Marekani ,Jebet Ng’etich ni wa kwanza katika msimamo wa kwa pointi 12,alama 4 zaidi ya Aisa.

Website |  + posts
Share This Article