Bangi ya thamani ya shilingi milioni 6 yanaswa Isiolo

Tom Mathinji
1 Min Read

Kikosi cha maafisa wa usalama kimenasa bangi ya thamani ya shilingi milioni 6 katika kaunti ya Isolo.

Operesheni hiyo ilitekelezwa baada ya maafisa hao kupata habari za kijasusi.

Kamanda wa polisi kaunti ya Isiolo Moses Mutisya, alisema kikosi hicho kilisimamisha gari katika eneo la Garbatula na kupata bangi hiyo.

Kulingana Mutisya, dereva wa gari hilo pamoja na abiria mmoja walitoroka Kupitia kichaka kilicho  Eldera area, na kuliacha gari hilo.

Alisema bangi hiyo ilikuwa ikisafiriahwa katika kaunti jirani.

Hata hivyo, aliongeza kuwa mwenye gari hilo anayeishi kaunti ya Meru amekamatwa na polisi na anasaidia kwa uchunguzi.

Mutisya alisema operesheni dhidi ya mihadarati na pombe haramu itaendelea.

TAGGED:
Share This Article