Kesi ya Lissu: Kizaazaa chashuhudiwa Kisutu

Viongozi kadhaa wa CHADEMA waliokuwa wamefika kufuatilia kesi dhidi ya Lissu walikamatwa na polisi.

Marion Bosire
1 Min Read

Kizaazaa kilishuhudiwa mapema leo nje ya mahakama ya Kisutu pale ambapo watu wengi walijitokeza kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi ya uhaini dhidi ya kiongozi wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu.

Maafisa wengi wa polisi walikuwa wamewekwa nje ya mahakama hiyo ya Kisutu kudhibiti hali ambapo maafisa wa chama hicho cha upinzani wanaripotiwa kutiwa mbaroni.

Kulingana na CHADEMA, makamu mwenyekiti wa chama hicho maeneo ya bara, John Heche, Chacha Heche mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mara na walinzi wawili walikamatwa na polisi.

CHADEMA imesema pia kwamba katibu mkuu wa chama hicho John Mnyika alikamatwa na polisi asubuhi katika eneo la Fire akielekea mahakamani Kisutu kufuatilia kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu.

Wengine waliokamatwa ni John Pambalu mkurugenzi wa Mafunzo, mipangilio na Uchaguzi, Twaha mwaipaya, Elizabeth Mambosho Katibu wa Chama Wilaya Ilala na Lucas Ngoto Mwenyekiti wa Chama kanda ya Serengeti.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu ambaye ameonyesha nia ya kugombea wa Urais wa Tanzania mwaka huu wa 2025 naye alizuiwa na Polisi kuingia Mahakamani Kisutu.

Website |  + posts
Share This Article