Serikali za kaunti zitapokea mgao wa shilingi bilioni 400.1 kwa mujibu wa bajeti ya mwaka 2024/25.
Hii ni asilimia 25.48 ya mapato halisi yaliyokusanywa na serikali kuu katika mwaka wa fedha wa 2020/21.
Serikali hizo zimekuwa mara kwa mara zikilalamikia uhaba wa fedha ambao zinasema umeathiri utoaji huduma kwa raia.
Hata hivyo, katika hatua inayoonekana kupiga jeki ugatuzi, serikali za kaunti pia zimetengewa fedha zaidi ambazo kima chake ni shilingi bilioni 44.4.
Fedha hizi zinajumuisha shilingi bilioni 8.76 ambazo ni mgao wa mapato kutoka kwa serikali kuu na shilingi bilioni 35.66 ambazo ni mkopo kutoka nje ya nchi.