Wawekezaji Konza wapewa miezi 18 kustawisha ardhi yao

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Ardhi Alice Wahome.

Serikali imetoa onyo kwa wawekezaji katika mji unaojegwa wa kiteknolojia wa Konza, kustawisha ardhi yao katika muda wa miezi 18 la sivyo ardhi hiyo itatwaliwa.

Alipozuru eneo hilo, Waziri wa Ardhi Alice Wahome alisema serikali itatwaa ardhi hiyo na kuiuza kwa wawekezaji wengine, iwapo wawekezaji waliopo kwa sasa hawastawisha ardhi yao.

Huku vipande vya ardhi 147 vikitolewa na zaidi ya vipande 100 kununuliwa, shinikizo zinaendelea kutanda kwa wawekezaji kuhakikisha wanajenga vipande vyao ili mji huo uanze kutumika.

“Mji wa kiteknolojia wa Konza umepewa kipaumbele na serikali, na hatutakubali wawekezaji kushikilia ardhi bila kustawisha. Kama hakutakuwa na maendeleo yoyote katika muda wa miezi 18 ijayo, tutatwaa ardhi hiyo na kuwapa wawekezaji wengine,” alisema Wahome.

Waziri Wahome alisema Mamlaka ya Taifa ya Ujenzi (NCA) pia inadhamiria kujenga taasisi ya kisasa ya utafiti na mafunzo katika mji wa Konza.

Aidha, kampuni ya umeme nchini, Kenya Power imesema itaanza shughuli ya kusambaza umeme katika mji huo kuanzia Ijumaa wiki hii ili kuhakikisha kila kipande cha ardhi kinapata umeme.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *