Mwanamuziki Kevin Kioko maarufu kama Bahati, hii leo ametoa wimbo uitwao “Umenipendelea” marudio ya wimbo “Umenipendelea” ulioimbwa na Henrick Mruma na Eliya Mwantondo.
Chini ya video ya wimbo huo ambayo alichapisha leo kwenye YouTube Bahati ameandika, “Yesu Mimi ni Mwenye Dhambi, Baba Mema unayonionyesha si Stastahili, Yesu umekua Babangu ata wakati siishi kama Mwanao. Yesu Umenipendelea!!!”.
Haya yanajiri saa kadhaa baada ya Bahati kuchapisha video kwenye Instagram ambapo anakiri kwamba yeye sio mkamilifu lakini kama binadamu kuna vitu ambavyo vinamzidi.
Aliendelea kulalamikia chuki ambayo amekuwa akipokea akisema inatoka kwa watu ambao anadhani wanaelewa Biblia, wanaojisingizia kuwa watu wa Mungu lakini wanadhihirisha wivu.
Mkewe Diana Bahati alimuunga mkono chini ya video hiyo akisema kwamba kibali hakina usawa na kwamba tasnia imejaa waovu wanaojifanya kuwa wakristo huku akisema kwamba Bahati ni nambari moja siku zote kwani Mungu alimchagua.
Vituko vya Bahati na mkewe vimekuwa vingi mtandaoni kuanzia kwa video ya wimbo wa dunia aliyochapisha iliyomwonyesha akichezewa densi na mwanadada mwenye makalio makubwa ambaye hakuwa amejisitiri.
Baadaye walichapisha video nyingine ambayo inamwonyesha Diana akitafuna chakula kisha kukiweka kwenye mdomo wa Bahati na nyingine ambayo anaonsha mguu wa Diana na kinywaji kisha ananikusanya kwenye glasi alafu anakunywa.
Vitendo vyao viliibua tetesi sana kati ya wanamitandao nchini huku wengi wakishangaa mfano ambao wawili hao wanatoa kwa wanao.
Msanii huyo alikemewa pia na wanamitandao kwa kutangaza sana wimbo alioimba kwa ajili ya kumuenzi waziri mkuu wa zamani Raila Odinga aliyefariki hivi maajuzi.
Wanamitandao walishangaa iwapo mwanamuziki huyo alikuwa anatumia kifo cha Raila kujinufaisha.
