Angola yajitosa kusuluhisha mzozo wa DRC

Dismas Otuke
1 Min Read

Angola imejitolea kuongoza mchakato wa kurejesha amani nchini DRC kwa kuongoza majadiliano  kati  ya waasi wa M23 na serikali ya DRC.

Taarifa kutoka kwa afisi ya Rais Joao Lourenco, imesema kuwa watawasiliana na waasi wa M23, ili kuwaita kwa mazungumzo mjini Luanda.

Mazungumzo hayo yatafanyika tarehe 18 mwezi huu,  huku pande zote mbili zikitarajiwa kushiriki.

Awali Rais Felix Tshisekedi, alikuwa ameapa kutozungumza na waasi wa M23, lakini ameonekana kulegeza msimamo na kuruhusu mazungumzo.

Haya yanajiri huku waasi wa M23 wanaoaminika kusaidiwa na serikali ya Rwanda, wakiwa wametwaa miji miwili mikuu mashariki mwa DRC;Goma na Kivu tangu Januari mwaka huu.

Maelfu ya  watu wameuawa tangu kuanza kwa mapigano kati ya wanajeshi wa serikali ya DRC na waasi wa M23.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article