Afrika Kusini yapokonywa pointi 3 safari ya kufuzu Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Harakati za Afrika Kusini kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao zimetiwa dosari baada ya kupokonywa alama tatu kwa kumjumuisha mchezaji asiyestahili katika mechi ya kundi C kufuzu dhidi ya Lesotho Machi 21 mwaka huu.

Uamuzi huo una maana kuwa Bafana Bafana wanashuka hadi nafasi ya pili kwa alama 14, katika kundi hilo wakiwa na uhaba wa magoli dhidi ya Benin wanaoongoza.

Afrika Kusini itawazuru Zimbabwe tarehe 10 mwezi ujao kabla ya kumalizia nyumbanio dhidi ya Rwanda siku nne baadaye katika mechi za  kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao.

 

Website |  + posts
Share This Article