Mabanati wa Kenya kurejea uwanjani leo dhidi ya miamba Korea Kombe La Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17 itarejea uwanjani leo usiku kwa mchuano wa pili wa kundi C, kuwania Kombe La Dunia dhidi ya Korea Kaskazini.

Kenya chini ya ukufunzi wa kocha Mildred Cheche ni sharti waepuke kushindwa mchuano huo wa kuanzia saa tano za usiku wa Jumapili,ili kuwa na matumaini ya kufuzu kwa robo fainali baada ya kupigwa na Uingereza magoli 2-0 katika pambano la ufunguzi.

Upande wao Korea wanalenga ushindi wa pili na kujikatia tiketi kwa awamu ya nane bora,baada ya kutitiga Mexico mabao 4-0 katika mchuano wa ufunguzi.

Share This Article