Achani apania kuboresha kilimo cha nazi Kwale

Achani amedokeza pia kuwa serikali ya kaunti hiyo imeanza kukarabati tingatinga za ukulima za kaunti hiyo ili kurahisishia wakulima wa Kwale kazi.

Marion Bosire
1 Min Read

Gavana wa Kwale Fatuma Achani amezindua zoezi la ugavi wa miche ya minazi 5,000 kwa wakulima 450 wa wadi 9 za kaunti hiyo.

Serikali ya Kwale imeendeleza juhudi za kuboresha kilimo kwa kugawa mbegu tofauti tofauti kwa wakulima kwa kaunti hiyo kila msimu ili kuhakikisha kuna utoshelevu wa chakula.

Wadi zitakazofaidika na miche hiyo ni pamoja na Tsimba-Golini, Mkongani, Kubo South, Ramisi, Kinondo, Bongwe-Gombato, Vanga, Dzombo na Kikoneni.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Achani amedokeza kuwa serikali ya kaunti hiyo sasa imeanza ukarabati wa tingatinga za ukulima za kaunti hiyo ili kurahisishia ukulima wakulima wa Kwale.

Naye Mwakilishi wadi wa Tsima Golini Mwachuo Mwaboza amewataka wakulima wataakao faidika na miche hiyo waweze kuitunza ili wafaidike na mimea hiyo katika siku za usoni.

Kwa upande wa wakaazi wakiongozwa na Karama Suleiman Pore na Marsela Maneno wamepongeza juhudi za serikali ya kaunti ya Kwale za kuboresha kilimo na kuwahimiza wakulima wenziwao kuzingatia mafunzo waliopatiwa na maafisa wa kilimo katika upanzi wa miche hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *