Maafisa wa Polisi wamemkamata mshukiwa wa wizi ya mananasi inayoshukiwa kuwa mali ya kampuni ya Del Monte.
Maafisa hao kutoka kituo cha polisi cha Ngoliba, walimkamata mshukiwa huyo akiwa na vipande 560 vya mananasikwenye operesheni iliyotekelezwa katika eneo la Kona Mbaya.
Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi Ngoliba, akisubiri kufikishwa mahakamani, huku mananasi hiyo iliyoibwa ikihifadhiwa kama ushahidi.
Kupitia ukurasa wake wa X, Huduma ya Taifa ya Polisi ilikariri kujitolea kukabiliana na wizi bidhaa za kilimo na kulinda uwekezaji wa ndani kote nchini.
Huduma hiyo ilitoa wito kwa wananchi kushirikiana na maafisa wa usalama kwa kutoa habari kuhusu vitendo vya kutiliw shaka.