Timu ya Taifa ya soka ya akinadada Harambee Starlets, itasafiri Jumamosi jioni kuelekea nchini Tanzania inakotarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya wenyeji mwezi Disemba.
Starlets wanatarajiwa kucheza mechi hizo mbili tarehe 1 na nne mwezi Disemba mtawalia, katika uwanja wa KMC Complex eneo la Mwenge, Jijini Dar es Salaam. Hata kabla ya safari hiyo, warembo hao wa hapa nyumbani walishiriki mazoezi yao ya kwanza.
Wachezaji watatu wa Ulinzi Starlets, Lorine Ilavonga, Bevaline Adika na Rasoha Siliya pamoja na mshambulizi wa Kibera Soccer Anna Arusi wamerejeshwa katika timu hiyo.
Wakati huo huo, mchezaji wa zamani wa Junior Starlets Judith Nandwa na mshambulizi wa Bandari Queens Happy Mutta, wakijumwishwa kwenye kikosi hicho kwa mara ya kwanza.
Starlets inatumia michuano hiyo ya kirafiki, kujiandaa kwa raundi ya tatu ya mechi za kufuzu kwa michezo ya Olimpiki dhidi ya Malawi Scorchers mwezi February mwaka 2027.