Nyota wa mieleka wa kulipwa wa WWEBronson Reed, aneaga dunia akiwa na umri wa miaka 38.
Mwanamieleka huyo ambaye jina lake halisi ni Jermaine Haley, aliaga dunia siku ya Ijumaa kutokana na matatizo ya kiafa, kulingana na shirika la World Wrestling Entertainment (WWE).
Kulingana na kampuni hiyo, Reed alikuwa mfanyakazi muungwana sana na aliyejali familia yake, huku akipendwa na wafanyakazi wenza.
Siku ya Ijumaa, mwanamieleka huyo alienziwa katika hafla ya WWE iliyofanyika Akins Ford Arena Jijini Athens, Georgia.
Wiki chache kabla ya kifo chake mwanamichezo huyo alipata majeraha mazito ikiwa ni pamoja na kuvunjika mbavu na jeraha la figo nchini Saudi Arabia baada ya kurushwa chini ya jukwaa na kupitia meza na Oba Femi wakati wa tukio la WWE.
Haley ni mwanamieleka wa pili kufariki katika muda wa miezi ya hivi majuzi, baada ya Benjamin Satterley, kufariki mwezi Septemba akiwa na umri wa miaka 40.