Ureno kumuenzi Ronaldo katika mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Denmark

Dismas Otuke
1 Min Read

Ureno itaandaa sherehe ya kipekee Jumamosi usiku kumuaga nahodha wake wa muda mrefu Christiano Ronaldo aliyestaafu wakati wa mechi yao ya jumamosi kuwania kombe la UEFA Nations League.

Shirikisho al soka barani Ulaya (UEFA) limeidhinisha kuwekwa kwa mabango ya picha na jezi nambari saba ambayo amekuwa akivalia Ronaldo ndani ya uwanja wakati wa mechi ya Jumamosi hidi ya Denmark.

Kila mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno atavalia jezi nambari saba katika mchuano wa leo kama njia moja ya kumuenzi Ronaldo aliye na umri wa miaka 41.

Ronaldo alitangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa  mapema mwezi huu  baada ya kufarakana na kocha wake Jorge Santos, alipomwacha nje katika mechi za mwzi uliopita za kuwania kombe la UEFA Nations League.

 

 

 

Share This Article