Arsenal huenda wakatawazwa mabingwa wa EPL Jumanne

The Gunners wangali kileleni pa jedwali kwa alama 82,kufuatia ushindi wa goli moja kwa bila nyumbani dhidi ya Burnley Jumatatu usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read
LONDON, ENGLAND - APRIL 25: Eberechi Eze of Arsenal celebrates scoring his team's first goal during the Premier League match between Arsenal and Newcastle United at Emirates Stadium on April 25, 2026 in London, England. (Photo by David Price/Arsenal FC via Getty Images)

Arsenal huenda wakatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza, EPL, siku ya Jumanne endapo wapinzani wa karibu Manchester City watakosa kupata ushindi ugenini dhidi ya Bournemouth.

The Gunners wangali kileleni mwa jedwali kwa alama 82 kufuatia ushindi wa goli moja kwa bila nyumbani dhidi ya Burnley Jumatatu usiku.

Bao la pekee na la ushindi lilipachikwa kimiani mwishoni mwa kipindi cha kwanza na Kai Haverts.

Manchester City wataitembelea Bournemouth katika mechi ya kufa kupona kwa timu zote mbili kuwania alama za ligi.

Wenyeji wanahitaji ushindi ili kuwa katika nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya au Europa League msimu ujao.

Man City ni sharti washinde ili kusalia kwenye kinyanga’nyiro cha ligi kuu na kulazimu mabingwa kubainika wakati wa mechi za kufunga msimu Jumapili hii.

Vijana wa Pep Guardiola wamo katika nafasi ya pili kwa alama 77 nao Bournemouth ni wa sita kwa pointi 55.

Share This Article