Chama cha The Equitable Party (TEP) kinachomilikiwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kimebadilishwa jina rasmi kuwa vugu vugu la Linda Mwananchi.
TEP kimebadilishwa jina wakati wa mkutano wa wajumbe (NDC) ulioandaliwa Ijumaa.
Aidha, mkutano huo uliafikiana juu ya masuala kadhaa ikiwemo nembo, rangi rasmi na makao makuu ya chama hicho.
Pia mkutano huo uliidhinisha vuguvugu hilo kutafuta ubia na vyama vingine vya kisiasa kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Mkutano huo uliandaliwa Ijumaaa faraghani.