Rais Ruto kuhutubia taifa Alhamisi usiku

Ingawa haijabainika bayana atakayoyazungumzia Rais, ajenda ya maendeleo ya kitaifa na hatua zilizopigwa na serikali yake  zinatarajiwa kutawala mazungumzo yake.

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa Alhamisi usiku kuanzia saa moja kupitia runinga zote humu nchini.

Hotuba hiyo ni ya kwanza baada ya muda mrefu na inajiri baada ya Rais kuaminika kufanya mazungumzo ya muda mrefu na Naibu wake Kithure Kindiki Jumatano usiku katika Ikulu ya Nairobi.

Ingawa haijabainika bayana atakayoyazungumzia Rais, ajenda ya maendeleo ya kitaifa na hatua zilizopigwa na serikali yake  zinatarajiwa kutawala mazungumzo yake.

Hotuba hiyo ya kitaifa pia inajiri wiki moja tu baada ya Rais Ruto kupokea ripoti kuhusu ukuaji wa kiuchumi na harakati za taifa kukua hadi kiwango cha mataifa ya kwanza kimaendeleo ulimwenguni.

Share This Article