Cameroon na Ghana wafungua WAFCON kwa ushindi

Awali, katika kundi hilo, Ghana maarufu kama Black Queens, waliwabwaga limbukeni Cape Verde 2-0 katika uga wa Moulay Rachid mjini Casablanca.

Dismas Otuke
1 Min Read

Cameroon na Ghana walifungua kipute cha Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake (WAFCON) kwa ushindi dhidi ya Mali na Cape Verde mtawalia Jumatano usiku nchini Morocco.

Marie Ngah aliwaweka kifua mbele Simba Marara wa Cameroon kifua mbele katika dakika ya 14 kabla ya Aissata Traore kusawazisha kunako dakika ya 30.

Ngah alirejea kwa goli la pili kwa penalti ya dakika ya 73 na kuwapa Cameroon ushindi katika mechi hiyo ya kundi D iliyosakatwa kiwarani Fes.

Awali, katika kundi hilo, Ghana maarufu kama Black Queens, waliwabwaga limbukeni Cape Verde 2-0 katika uga wa Moulay Rachid mjini Casablanca.

Doris Boaduwaa alipachika bao la kwanza ndani ya dakika sita pekee za mchezo akiunganisha pasi ndefu yake Portia Boakye, kabla ya Eleia Vieira kujifunga mwanzoni mwa kipindi cha pili na kuwapa Ghana ushindi huo maridhawa uliowawezesha kuongoza kundi hilo kwa alama tatu sawa na Cameroon yenye uhaba wa magoli.

Share This Article