Kenya Power yarejesha umeme kufuatia hitilafu

Kulikuwa na nuru gizani baada ya umeme kurejea majira ya saa tano unusu jana usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya umeme nchini ya Kenya Power imetangaza kurejesha umeme katika maeneo yote yaliyoathirika jana Jumatano usiku.

Kulikuwa na nuru gizani baada ya umeme kurejea majira ya saa tano unusu jana usiku.

Maeneo ya Nairobi, Pwani na Mlima Kenya pamoja na maeneo kadhaa ya katikati mwa Bonde la Ufa yalikumbwa na kukatika kwa umeme Jumatano jioni.

Hali hiyo iliwaacha wakazi kwenye giza totoro huku shughuli na biashara zinazotegemea umeme zikikwama kwa kipindi kirefu.

 

Share This Article