Angalau watu sita wamefariki na wengine watatu kuokolewa baada ya jumba moja lililokuwa likijengwa kuporomoka huko Syokimau kwenye barabara ya Mombasa Road.
Mkasa huo umetokea wakati sehemu ya jumba hilo lenye ghorofa tisa ilipoporomoka.
Kamanda Polisi kaunti ya Nairobi Issa Mohamud amesema miili mitatu imeopolewa wakati pirikapirika za kuwaokoa manusura wote wakiwa wanaume wa umri wa makamu zikiendelea.
Aliongeza kuwa wafanyakazi wengine watano waliokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu na kundi la zimamoto kutoka kaunti ya Nairobi wamepelekwa katika eneo la mkasa kuongoza shughuli uokoaji.
Mkasa huo unatokea wiki kadhaa baada ya jumba jingine kuporomoka mtaani Eastleigh na kuwaua watu wanane.