Mchuano wa magwiji wa klabu ya Arsenal na magwiji wa Harambee Stars uliokuwa uchezwe leo usiku katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo umeahirishwa.
Kulingana na taarifa kwa umma, wengi wa magwiji wa Arsenal walishindwa kusafiri kwa wakati kwa ajili ya mechi hiyo.
Hata hivyo, afueni ni kuwa waandalizi wameahidi kurejesha pesa za wote waliokuwa wamenunua tiketi.
Tiketi za mchuano huo zilikuwa zikiuzwa kwa kati ya shilingi 500 hadi 20,000.