Watu wanne wanaswa na kilo 454 za mihadarati Msambweni

Msako zaidi ulifanywa na polisi mtaani Ganja katika kata ya Kinondo waliponasa magari mawili na pikipiki moja.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa polisi  wa Kenya wakishirikiana na wale wa Tanzania,wamewanasa watu wanne eneo la Msambweni,kaunti ya Kwale wakiwa na kilo 454 za mihadarati inayokisiwa kuwa ya kima cha shilingi bilioni 3.6.

Walanguzi hao walipata kufuatia msako uliofanywa katika mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Lungalunga-Horohoro tarehe 5 mwezi huu.

Baada ya washukiwa hao kutiwa mbaroni waliowaongoza polisi hadi kijiji cha Shirazi eneo la Msambweni kwa mshukiwa wa pili.

Msako zaidi ulifanywa na polisi mtaani Ganja katika kata ya Kinondo waliponasa magari mawili na pikipiki moja.

Washukiwa hao wamewekwa korokoroni wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Polisi wamepongeza ushirikiano wa maafisa wa Kenya na wenzao wa Tanzania kwa ufanisi huo.

Share This Article