Rais wa Israel Isaac Hergoz amemteua Gadi Eisenkot,mpinzani mkuu wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu,kujaribu kuunda serikali mpya.
Netanyahu anajaribu kunusuru uongozi wake wa muda mrefu kwa kujaribi kushawishi uungwaji mkono kutoka kwa wabunge wa mpinzani wake baada ya chama chake cha kidini kukosa kupata wingi wabunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 27.
Endapo Eisenkot atafanikiwa kupata uungwaji mkono kutoka kwa wabunge wa Netanyahu ,basi atashika hatamu za Waziri mkuu .
chama cha upinzani cha Eisenkot kilizoa viti 48 kati ya 120 katika bunge la israel huku Netanyahu akipata wabunge 53 ,wote wakikosa wingi unaohitajika kubuni serikali.
Eisenkot anakabiliwa na changamoto kadhaa katika kuunda serikali mpya ,ikiwemo kugawana mamlaka na Netanyahu.