Mahakama imemhukumu Vincent Odhiambo kifungo cha miaka 10 gerezani au faini ya shilingi milioni 24, baaada ya kupatikana na hatia ya ulanguzi wa mihadarati.
Kupitia kwa taarifa, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP). ilisema Odhiambo alishtakiwa chini ya sehemu ya 4(a)(ii) ya sheria za kudhibiti ulanguzi wa mihadarati ya mwaka 2022.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Felix Namasake, uliambia ahakama kuwa mnamo Januari 18, 2026, katika barabara ya Kapchorwa-Torongo Murram, kaunti ndogo ya Keiyo Kusini, kaunti ya Elgeyo Marakwet County, Odhiambo pamoja na wenzake walipatikana na kilo 266.2 za bangi za thamani ya shilingi 7,986,000, zikiwa ndani ya gari aina ya Toyota Fielder.
Kwenye kesi hiyo, upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi sita, huku mahakama ikithibitisha ushahidi uliotolewa na kutoa hukumu dhidi ya mwanamume huyo.
Afisi ya DPP, ilisema mahakama ilimpa mshtakiwa kifungo hicho ili kulinda umma dhidi makosa sawa na hilo.