Omar: Kenya ina mazingira bora ya biashara

Omar alidokeza kuwa diplomasia ya Kenya ni nguzo kuu katika sera za mambo ya nje ya taifa hili.

Tom Mathinji
1 Min Read
Hassan Omar - Katibu Mkuu wa chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Katibu Mkuu wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) Hassan Omar, amesema Kenya imejitolea kuhakikisha mazingira bora ya biashara, kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Akizungumza alipohudhuria maonyesho ya bidhaa ya Sri Lanka Jijini Nairobi, Omar alidokeza kuwa diplomasia ya Kenya ni nguzo kuu katika sera za mambo ya nje ya taifa hili, hususan katika kufanikisha ukuaji wa viwanda, biashara, uwekezaji na maendeleo endelevu.

Kwenye maonyesho hayo, Omar alielezea umuhimu wa ushirikiano wa mataifa ya kusini ili kuboresha maslahi ya pamoija, biasharana uwekezaji wa pamoja, upanuzi wa soko na kushughulikia changamoto za kibiashara miongoni mwa nchi zinazostawi.

Omar, alihutubia mkutano huo kwa mwaliko wa balozi wa Sri Lanka hapa nchini Ruvini De Silva.

Share This Article