Rwanda,Madagascar,Zambia,Tunisia na Uganda wafungua raga ya vipusa Afrika kwa ushindi

Jumla ya mataifa 11 yanashiriki mashindano hayo yatakayokamilika Jumapili, huku mshindi akifuzu kwa mashindano ya msururu wa  HSBC Sevens divisheni ya tatu mwaka ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rwanda ,Madagascar,Tunisia ,Zambia,Uganda na Afrika Kusini wameanza mashindano ya  raga Afrika kwa wanawake kwa ushindi siku ya Jumamosi katika uwnaja wa RFUEA ,jijini Nairobi.

Madagascar wameshinda mechi mbili za kundi C wakiishinda Mauritius pointi 12-5, kabla ya kuwalemea Burkina Faso alama 36-12.

Uganda iliwabwaga Burkina Faso  alama 45-0,nao Tunisia wakaicharaza Ghana 21-0, nao Zambia wakainyofoa Zimbabwe 36-5.

Mabingwa watetezi Afrika Kusini wameanza kutetea taji hiyo kwa ushindi wa  57-0.

Jumla ya mataifa 11 yanashiriki mashindano hayo yatakayokamilika Jumapili, huku mshindi akifuzu kwa mashindano ya msururu wa  HSBC Sevens divisheni ya tatu mwaka ujao.

Share This Article