Afrika itawakilishwa na timu 10 katika makala ya 23, ya fainali za Kombe la Dunia, ziatazoanza rasmi Juni 12 katika mataifa ya Marekani,Canada na Mexico.
Timu 48 zinashiriki kwa mara ya kwanza huku pia idadi ya timu za Afrika ikiongozeka maradufu kutoka 5 hadi 10.
Morocco iliyocheza hadi nusu fainali mwaka 2022, inaongoza timu za Afrika katika kipute hicho.
DRC inarejea katika fainali hizo baada ya subira ya miaka 52, nao Cape Verde, wamefuzu kwa mara ya kwanza.
Tunisia,Algeria,Misri,Senegal,Afrika Kusini,Ghana na Ivory Coast pia zitashiriki.
Zimesalia siku 28 kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia.