Wapiga kura wa Emurua Dikirr wamchagua mbunge mpya

Jumla ya vituo 94 vya kupigia kura vimetengwa katika maeneo mbalimbali, huku kituo kikuu cha ujumuishaji kikiwa Emurua Dikirr Technical Training .

Dismas Otuke
1 Min Read

Wapiga kura wapatao 44,353, wa Emurua Dikirr, wanatarajiwa kujitokeza leo Alhamisi Mei 14, kumchagua Mbunge mpya.

Uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia kifo cha Johana Ng’eno, Februari 28, kupitia mkasa wa ajali ya ndege akiwa na watu wengine watano.

Waliojitosa ulingoni kuwania kii hicho ni; David Keter wa chama cha UDA, Vincent Rotich wa chama cha DCP, Gideon Koech wa NVP, Desmas Cherono kutoka PNU na Kenneth Kiprono wa RLP.

Wakazi wamestahimili baridi kali ya asubuhi na kujitokeza mmoja baada ya mwingine kuanzia saa kumi na mbili asubuhi kutekeleza haki yao ya kidemokrasia.

Jumla ya vituo 94 vya kupigia kura vimetengwa katika maeneo mbalimbali, huku kituo kikuu cha ujumuishaji kikiwa Emurua Dikirr Technical Training .

Share This Article