Wakenya waadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Raila

Jumatano jioni ibada ya kuwasha mishumaa kwenye kaburi lake iliandaliwa kutangulia ukumbusho wa leo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ni mwaka mmoja tangu aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga alipoaga dunia nchini India akipokea matibabu.

Familia ndugu jamaa na rafiki wanatarajiwa kukongamana nyumbani kwa hayati Raila,Kang’o ka Jaramogi, katika kaunti ya Siaya, kufanya ibada ya ukumbusho.

Jumatano jioni ibada ya kuwasha mishumaa kwenye kaburi lake iliandaliwa kutangulia ukumbusho wa leo.

Naibu mwenyekiti wa chama cha ODM kilichoanzishwa na marehemu Raila,Otiende Amollo, alionya kuwa kamwe hawatakubali siasa kwenye ibada ya Alhamisi.

Amollo aliwataka wote watakaohudhuria ibada kujiepusha na siasa.

Mwezi wa Oktoba umetengwa kwa ajili ya kumkumbuka Raila ambaye ni mmoja wa wanasiasa waliopigania demokrasia na haki za kibinadamu.

Share This Article