Kazi ipo, Kenya ikivaana na Morocco leo kipute cha AFCON

Mechi hiyo ya kundi B dhidi ya miamba Morocco, utakuwa mtihani mkubwa kwa Kenya ,kutokana na tofauti kubwa ya maendeleo ya kimchezo kati ya nchi hizo mbili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Baada ya subira ya miaka na mikaka, hatimaye mabarubaru wa Kenya chini ya umri wa miaka 20, Rising Stars, watacheza mechi ya kwanza katika historia kuwania kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), leo usiku nchini Misri.

Hata hivyo, mechi hiyo ya kundi B dhidi ya miamba Morocco, utakuwa mtihani mkubwa kwa Kenya inayonolewa na Salim Babu, kutokana na tofauti kubwa ya maendeleo ya kimchezo kati ya nchi hizo mbili.

Pambano hilo litasakatwa katika dimba la 30 Juni Air Defence jijini Cairo, kuanzia saa tatu usiku na litatanguliwa na mchuano kati ya mabingwa mara saba, Nigeria, dhidi ya Tunisia  saa kumi na mbili jioni.

Mechi ya pili kwa Kenya itakuwa dhidi ya Tunisia Jumapili hii, na hatimaye kufunga ratiba ya kundi B dhidi ya vigogo Nigeria Mei 7.

Katika mechi za jana kundini A, Sierra Leone, ili wagutusha wenyeji Misri, ilipowanyuka mabao 4-1 huku Afrika Kusini, ikiibwaga Tanzania, goli moja bila jawabu.

Timu nne bora mashindanoni zitafuzu kushiriki Kombe la Dunia nchini Chile kati ya Septemba na Oktoba mwaka huu.

Website |  + posts
Share This Article