5 wafariki, wengine wajeruhiwa kwenye ajali Kitui Kusini

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara ya Ikutha–Mutomo katika eneo bunge la Kitui Kusini, kaunti ya Kitui.

KBC Digital News
1 Min Read

Watu 5 wamefariki baada ya dereva wa lori walimokuwa wakisafiria kushindwa kulidhibiti na lori hilo kubingiria mara kadhaa.

Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali za Ikutha na Mutomo ili kupokea matibabu.

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara ya Ikutha–Mutomo katika eneo bunge la Kitui Kusini, kaunti ya Kitui.

Akithibitisha ajali hiyo, Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Ikutha Raphael Mutiso alisema lori hilo lilikuwa limebeba wafanyabiashara dereva wake aliposhindwa kulidhibiti na kubingiria mara kadhaa.

Mutiso ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wanapotumia barabara hiyo ambayo kwa sasa inakarabatiwa.

 

Share This Article