Saudi Arabia imewafurusha wahamiaji 14,905 haramu katika msako wa wiki moja unaondeshwa kukabiliana na uhamiaji haramu.
Msako huo ulifanywa kati ya Agosti 20 na 26 ambapo watu 14,434 wlikamatwa na kufurushwa.
Ethiopia ndio yenye idadi kubwa ya wahamiaji haramu nchini Saudi Arabia, ikifuatwa na Yemen.
Saudi Arabia imesema watu hao waliofurushwa wanaishi na kufanya kazi nchini humo bila vibali.
Maelfu ya wahamiaji wangali wanapigwa msasa kabla ya kurejeshwa makwao.