Papa Leo wa 14 aendelea kupokea nafuu hospitalini baada ya upasuaji

Papa anatarajiwa kusalia hospitalini kwa juma moja huku akifutilia mbali zaira zake rasmi alizokuwa amepanga hadi Oktoba 20.

Dismas Otuke
1 Min Read
Papa Francis.

Papa mtakatifu Leo wa 14 anaendelea kupata nafuu kufuatia upasuaji wa kufana aliofanyiwa kuondoa uvimbe wa saratani kwenye mapafu yake ya kulia.

Kulingana na Vatican, Papa aliye na umri wa miaka 71, alifanyiwa upasuaji uliofanikiwa Jumanne wiki hii katika hopsitali ya Gemelli mjini Rome.

Madaktari waliesema waliondoa sehemu ya chini ya mapafu yake bila matatizo yoyote .

Uvimbe huo ulibainika wakati Papa alikuwa akifanyiwa uchunguzi wa kila mara wa kimatatibabu.

Papa anatarajiwa kusalia hospitalini kwa juma moja huku akifutilia mbali zaira zake rasmi alizokuwa amepanga hadi Oktoba 20.

Share This Article