Ruto atoa hakikisho la Kenya kuandaa mashindano bora ya Dunia mwaka 2029

Kenya itaandaa mashindano hayo ya Dunia  yatakayokuwa makala ya 22 ,mwezi Septemba  mwaka 2029,katika uwanja wa Kasarani .

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ametoa hakikisho la Kenya kuandaa mashindano bora ya Riadha Duniani mwaka 2029,baada ya kutwikwa jukumu hilo mwezi uliopita.

Ruto alisema hayo Jumatano jioni alipokutana na Rais wa Shirikisho la Riadha ulimwenguni Lord Sebatian Coe, katika Ikulu ndogo ya Eldoret, kaunti ya Uusin Gishu .

Alisema  kuwa ukarabati unaofanyiwa uwanja wa Kasarani ambao utaandaa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwakani na baadaye pia kukarabatiwa kwa mashindano ya Riadha duniani mwaka 2029.

Ilikuwa ziara ya kwanza kwa Seb Coe humu nchini tangu Kenya kuishinda miji ya Rome,na London mwezi uliopita,na kutangazwa kuwa mwandalizi wa mashindano hayo ya dunia yatakayofanyika Afrika kwa mara ya kwanza.

Kenya itaandaa mashindano hayo ya Dunia  yatakayokuwa makala ya 22 ,mwezi Septemba  mwaka 2029,katika uwanja wa Kasarani .

Seb Coe aliwasili nchini Kenya mapema Jumatano na kuwahutubia wanahabari kabla ya kufunga safari kwenda Eldoret kwa kikao na Rais Ruto.

Coa aliandamana na  Afisa Mkuu wa shirikisho la Riadha Ulimwenguni Jon Ridgeon.

Share This Article