Wanaogema na kuuza pombe haramu mashakani

Naibu Rais Kithure Kindiki amedokeza kuwa vita dhidi ya vinywaji hatari vimeimarishwa na hakuna atakayesazwa kuhakikisha hakuna Mkenya anapewa semu kwa kisingizio ni mvinyo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki kwenye ziara katika eneo bunge la Limuru, kaunti ya Kiambu.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, ametoa onyo kali dhidi wanaouza pombe haramu, akisema watakamatwa na kuwajibiki maisha has issued a warning to sellers of harmful alcoholic drinks, declaring that they will be arrested and made to account for putting the lives of Kenyans at risk.

Kindiki alidokeza kuwa vita dhidi ya vinywaji hatari, vimeimarishwa na hakuna atakayesazwa kuhakikisha hakuna Mkenya anapewa semu kwa kisingizio ni mvinyo.

“Nawaonya wale wanaouza vinywaji hatari, kwamba siku zao zinakaribia. Nawahakikishia kuwa hatutamkubalia yeyote kuuza vinywaji hatari kwa kisingizio ni pombe,” alisema Kindiki.

Kindiki alisema atakabiliana na wanaouza pombe haramu, jinsi alivyokabiliana na majangili alipokuwa Waziri wa Usalama wa Taifa.

“Wengine hata hawana mahala maalum pa kufanya biashara. Wanachanganya tu kemikali na kuwauzia Wakenya. Tumekabiliana na Alshabab na majangili, hatuwezi shindwa na wafanyabiashara wa pombe haramu,” alidokeza Kindiki.

Aliyasema hayo Ijumaa katika eneo bunge la Limuru, kaunti ya Kiambu alipozindua vifaa vya kuhifadhi maziwa vya vyama kadhaa vya ushirika.

Share This Article