Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), imefaulu kutupiliwa mbali kwa ombi lililowasilishwa na Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi, kuzuia kutwaliwa kwa shilingi milioni 813.1, zinazohusishwa na utoaji ghushi wa zabuni za ujenzi wa barabara.
Kesi hiyo inahusiana na malipo kwa kampuni tano zilizopewa zabuni za ujenzi wa barabara na Halmashauri ya Barabara za Mijini (KURA), Halmashauri ya Barabara za Mashinani (KeRRA) na Halmashauri ya Barabara Kuu (KeNHA).
Kulingana na EACC, Wamatangi, alipokuwa akihudumu wadhifa wa Seneta wa Kiambu, alitumia wadhifa huo kushawishi kampuni alizohusishwa nazo kupata zabuni hizo, na kwamba stakabadhi bandia ziliztumika kupata zabuni hizo.
“Tume hii inataka kutwaliwa kwa shilingi 813,145,532.40 kutoka kwa mshtakiwa pamoja na wenzake,na pia kutwaliwa kwa fedha zilizo kwenye akaunti za benki za kampuni hizo,” ilisema EACC kupitia ukurasa wa X.
Mahakama ilishikilia kuwa wadhifa wa ubunge hauna kinga dhidi ya uvunjaji wa sheria.