Ethiopia na Eritrea zimekata uhusiano wa Kidiplomasia baada ya Ethiopia kuishutumu Eritrea kwa kuhusika na vita vilivyoanza upya katika eneo la Trigray.
Wizara ya mambo ya kigeni nchini Ethiopia ilikuwa ya kwanza kutangaza kufunga ubalozi wake nchini Eritrea, kabla ya Eritrea kujibu kwa kumwondoa balozi wake mjini Adis Ababa na kufunga ubalozi huo.
Ubalozi wa Ethiopia nchini Eritrea ulifunguliwa tangu mwaka 2018, kama njia ya kurejesha uhusiani kati yake na Eritrea baada ya kushinda tuzo ya amani ya Nobel.