Rais Ruto atoa hatimiliki za ardhi Mombasa

Hatimiliki hizo ni miongoni mwa hatimiliki 300,000, ambazo serikali imetoa wiki hii kwa wakazi wa ukanda wa pwani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ambaye angali ziarani katika eneo la Pwani, ameongoza shughuli ya utoaji hatimiliki ya ardhi katika eneo la Mama Ngina Waterfront Gardens katika kaunti ya Mombasa.

Rais ametoa jumla ya hatimiliki 5,000 kwa wakazi wa maeneo ya Dongo Kundu, Waitiki, Mwakirunge, Mikindani na Mafisini.

Hatimiliki hizo ni miongoni mwa hatimiliki 300,000 ambazo serikali imetoa wiki hii kwa wakazi wa Pwani.

Akiwa ziarani Pwani siku ya Ijumaa, Rais pia amezindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo chuo cha kiufundi cha Watamu, soko la kisasa la Watamu na mradi wa uunganishaji umeme katika shule ya Rare, kaunti ya Kilifi.

Aidha, aliweka jiwe la msingi la mabweni ya taasisi ya Godoma eneo la Matano Manne.

Pia Rais alizundua ujenzi wa barabara ya umbali wa kilomita 13 Gede-Kakuyuni katika eneo la Mijomboni eneo bunge la Kilifi kaskazini kwa gharama ya shilingi bilioni 1.

Share This Article