Mombasa United FC yaipiku Kariobangi Sharks

Mechi ya marudio itapigwa Oktoba 10 huku mshindi wa jumla akifuzu kucheza ligi kuu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mombasa United FC imeibwaga Kariobangi Sharks  mabao 2-1 katika duru ya kwanza  ya mchujo wa kushiriki Ligi Kenya  msimu wa mwaka 2026/2027 ,mechi iliyopigwa katika kaunti ya Mombasa siku ya Alhamisi.

Mechi ya marudio itapigwa Oktoba 10 huku mshindi wa jumla akifuzu kucheza ligi kuu.

Sharks walimaliza nafasi ya 16 katika ligi kuu msimu jana wakati Mombasa United wakimaliza nafasi ya tatu katika ligi ya NSL msimu uliopita.

Share This Article