Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, amesema ujenzi wa uwanja wa michezo wa Ruring’u kaunti ya Nyeri, utagharimu shilingi milioni 900.
“Uwanja wa Ruring’u ni mojawepo wa viwanja 32 ambazo zinajengwa kote nchini, ili kupiga jeki uwanja wa Kasarani, ule wa Nyayo na Talanta, kuimarisha michezo hapa nchini,” alisema Kindiki.
Akizungumza alipokagua ujenzi wa uwanja huo katika kaunti ya Nyeri leo Ijumaa, Kindiki alisifu kazi ya ukarabati inayoendelea kwenye uwanja huo, akisema ujenzi wake umekamilika asilimia asilimia 70.
Wakati huo huo, Kindiki pia alikagua ujenzi wa soko la kiuchumi la Asian Quarters, utakaogharimu shilingi milioni 324, likitarajiwa kuwahifadhi wafanyabiashara 750.
Walioandamana na Kindiki kwenye ukaguzi huo ni pamoja na Seneta wa Nyeri Wahome Wamatinga, wabunge Dancun Mathenge ( Nyeri Mjini), Eric Wamumbi ( Mathira), Njoroge Wainaina (Kieni), Wawakilishi wadi, miongoni mwa wengine.