Milipuko imesikika katika Jiji Kuu Addis Ababa, Ethiopia, huku mapigano makali yakiendelea kati ya jeshi la serikali na muungano wa makundi yenye silaha.
Kulingana na vyanzo vya habari nchini humo, milipuko hiyo ilitokea Alhamisi, saa chache baada ya serikali ya Ethiopia kupiga marufuku ndege zisizo na rubani kupaa katika Jiji hilo na maeneo yaliyo karibu.
Mashambulizi hayo yanadaiwa kutekelezwa katika Jiji la Addis Ababa, huku mashambulizi mengine yakielekezwa katika Makao Makuu ya jeshi.
Utawala nchini humo haujatoa taarifa kuhusu milipuko hiyo inayodaiwa imetekelezwa na muungano huo wa makundi yenye silaha, kwa lengo la kumuondoa mamlakani Waziri Mkuu Abiy Ahmed.
Makundi hayo yenye silaha ni pamoja na Tigray People’s Liberation Front (TPLF) na makundi kutoka maeneo ya Amhara, Afar, Somali na Benishangul-Gumuz.