Mabingwa wa Afrika mwaka 2024 Ivory Coast, almaarufu The Elephants, watashuka uwanjani Dalllas leo Jumanne usiku kukabiliana na Norway katika mechi ya tano ya raundi ya 32.
Mchuano huo utaanza saa mbili usiku ikiwa mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana katika Kombe la Dunia.
Sadfa ni kuwa mataifa hayo pia yalimaliza ya pili kutoka kwa makundi yao, Ivory Coast ikimaliza ya pili kundini E baada ya kuwashinda Ecuador kwa bao moja, ikapoteza 2-1 dhidi ya Ujerumani na kuwalaza Curasao 2-0.
Norway pia ilichukua nafasi ya pili kundini I ikiwachraza Iraq 4-1, ikawalemea Senegal 3-2, na hatimaye kupoteza 4-1 dhidi ya Ufaransa.
Norway inayojivunia mfungaji bora katik Ligi Kuu Uingereza msimu uliopita Erling Halaand ni ya 31 Duniani huku Ovory Coast ikishikilia nafasi ya 33.
Mshindi wa ngarambe hiyo ataweka miadi ya kukabiliana na Brazil katika raundi ya 16 bora.