Maafisa wa polisi kutoka vitengo mbalimbali wamenasa lita 3,600 za pombe haramu na kuharibu vifaa vya kutengezea pombe katika msako ulioendeshwa siku ya Jumatano.
Msako huo ulifanywa kwa pamoja na polisi kutoka Huduma ya Kitaifa ya Polisi, NPS, maafisa wa utawala na wale wa Mamlaka ya Kupambana na Pombe na Mihadarati (NACADA).
Yamkini biashara hiyo haramu imekuwa ikiendeshwa katika kaunti ndogo za Marsabit Central na Sagante-Jaldesa katika taarafa za Nagayo, Sagante, na Badasa.
Aidha, polisi wamewataka wananchi kutoa taarifa kuhusu wanaogema na kuuza pombe haramu ili kukomesha uovu huo.